
![]()
Jamii
Ukurasa huu unayo habari ya kukusaidia kung'amua kuhusu nafasi na makazi yanayofanyika katika jamii yenyeji pale unakoishi
Mabaraza Yenyeji
Kwa watu wanaoishi Riding Mashariki ya Yorkshire (ikiwa sio pamoja na walio ndani ya jiji la Hull), jamii tawala ni Riding Mashariki ya Baraza la Yorkshire. Wanatoa huduma mbalimbali kwa wakaazi wenyeji, na waweza saidia kwa njia nyingi. Jinsi ya kuwasiliana nao ipo hapa chini.
Kwa watu walioko ndani ya mipaka ya jiji la Hull, jamii yenyeji tawala ni Baraza la Jiji la Hull. Wanatoa huduma za namna mbalimbali kwa wakaazi wenyeji, na waweza saidia kwa njia nyingi.
Maktaba
Tafadhali wasiliana na Baraza lako lenyeji kwa habari kuhusu huduma za maktaba katika sehemu yako (kwa mfano: mahali zilipo, masaa ya kufungua, au nafasi)
Usafiri wa Jamii
Mabaraza yenyeji yaweza kutoa habari kuhusu juhudi za usafiri wa mashinani - zingine kati yake ambazo zaweza kugharamiwa na baraza.
Tafadhali zingatia kwamba mipango mingine ya usafiri wa jamii yaweza kuwa sio ya kila mtu, kwa mfano yaweza kutumiwa tu na watu walio na shida za usabili.
| Kuweza kuwasiliana na Riding Mashariki ya Baraza la Yorkshire: tafadhali piga simu 01482 393 939 na sema tu "Swahili" ili wajue wahitaji mkarimani wa Kiswahili ili kuendelea na swala lako. |
Kuwasiliana na Baraza la Jiji la Hull: Tafadhali piga simu 01482 300 300 na sema tu "Swahili" kuonyesha yakwamba wahitaji mkarimani wa Kiswahili ili kuendelea na swala lako. |