
Afya
Ukurasa huu utakusaindia katika kung'amua kuhusu huduma za afya zilizo karibu nawe na habari juu ya hali mahususi za utibabu.
Huduma ya Afya ya Taifa (NHS)
Huduma ya Afya ya Taifa ina jukumu la kutoa utunzi wa afya kwa waishio Uingereza. Kwa habari zaidi tafadhali wasiliana na ‘NHS Direct' (ona hapa chini)
Madaktari/ Hospitali/ Madaktari wa Macho/ Madaktari wa Meno / Maduka ya Madawa
Kutafuta daktari wa karibu (GP), hospitali, daktari wa macho, daktari wa meno au duka la dawa tafadhali wasiliana na ‘NHS Direct' (ona hapa chini)
Hali ya Afya
Kwa habari au mawaidha kuhusu hali yoyote ya afya (kwa mfano saratani (kansa), ugojwa wa sukari, ugojwa wa moyo) tafadhali wasiliana na ‘NHS Direct' (ona hapa chini)
Magojwa Madogo (madawa ‘ya kutolewa kwa dirisha')
Kama uko na homa au koo linalowasha, huwa kawaida sio sharti umuone daktari kwa matibabu. Kunazo dawa nyingi za nyumbani au dawa za ‘kutolewa dirishani' na amazo zaweza kuondoa ishara kama vile pua majimaji. Wasiliana na ‘NHS Direct (ona hapa chini) kwa mawaidha kuhusu dawa za nyumbani ambazo waweza kujaribu (kama vile kuvuta mvuke wa maji ya kuoga) au bidhaa anbazo waweza kununua (kama vile dawa za koo) kukusaindia kujisikia nafuu. Pia waweza kukupa mawaidha kama ni sharti uende kutafuta mawaidha ya kiafya kutoka kwa daktari.
Afya ya Akili
Kwa habari juu ya Huduma za Afya ya Akili katika sehemu yako, tafadhali wasiliana na ‘NHS Direct' (ona hapa chini)
Afya ya Ungono
‘NHS Direct' waweza kutoa habari na mawaidha kuhusu mambo mengi ya afya ya ungono - uja uzito, madawa ya kuzuia uja uzito, kutoa mimba, kutokwa na mimba, magonjwa ya ungono na kadhalika. Pia waweza kutoa habari kuhusu huduma za afya ya ungono zinazopatikana karibu na mahali unapoishi. (Jinsi ya kuwasiliana nao hapa chini)
Ulemavu wa Dawa au pombe/ Uvutaji Sigara
‘NHS Direct' (ona hapa chini) waweza kutoa habari na mawaidha kuhusu ulemavu wa dawa au pombe, ikiwa ni pamoja na ni huduma gani zenyeji zinazopatikana kusaindia watu kukabiliana na ulemavu huu.
Waweza pia kutoa habari na mawaidha kwa watu wanaotaka kuacha kuvuta sigara.
Wasiliana na ‘NHS Direct' katika simu 0845 46 47- sema tu "Swahili" kuonyesha yakwamba unahitaji mkarimani wa Kiswahili ili kuendelea na mazungumzo.
|