

Kunayo makundi mengi ya watu tofauti wanaoishi mle Riding ya Mashariki ya Yorkshire na Hull - kwa mfano: watoto, watu wazima Ngubaru, wazazi, walemavu, au watunzaji kutaja wachache tu.
Hapa chini ni habari ambayo yaweza kuwa ya manufaa kwa baadhi ya makundi haya:
Watunzaji
Kama unatunza mtu aliye mgonjwa au mwenye ulemavu, waweza kupata msaada na auni kutoka kwa Baraza lako lenyeji:
Watoto/Vijana
Mabaraza yenyeji yaweza kukupa habari kuhusu huduma za watoto, ikiwa ni pamoja na chekechea na vilabu vya vijana. Baraza pia laweza kutoa habari kuhusu huduma za watoto ambazo zinatolewa na mashirika mengine yenyeji.
Watu Walemavu
Kama uko na ulemavu (wa kimwili, wa ufahamu au wa hisiya) basi Mabaraza yenyeji yaweza kutoa huduma mbalimbali kukusaindia, kwa mfano vituo vya kukaa mchana kutwa, linganisho za nyumbani, auni, nyumba za makaazi au kwa kutoa nishani za uwezekaji magari za walemavu.
Watu Wazima Ngubaru
Kuna huduma nyingi kwa watu wazima ngubaru zinazopatikana kutoka kwa Baraza lenyeji, kwa mfano utunzaji katika makaazi, msaada wa kinyumbani, ‘milo juu ya gurudumu', na linganisho za nyumbani.
Wazazi
Kama wewe ni mzazi waweza ng'amua kuhusu huduma za familia kutoka kwa Baraza lako lenyeji, kwa mfano auni ya wazazi au ya utunzaji wa watoto.
| Kuweza kuwasiliana na Riding Mashariki ya Baraza la Yorkshire: tafadhali piga simu 01482 393 939 na sema tu “Swahili” ili wajue wahitaji mkarimani wa Kiswahili ili kuendelea na swala lako. |
Kuwasiliana na Baraza la Jiji la Hull: Tafadhali piga simu 01482 300 300 na sema tu “Swahili” kuonyesha yakwamba wahitaji mkarimani wa Kiswahili ili kuendelea na swala lako.