
Masilahi
Ukurasa huu unayo habari ambayo itasaindia watu na mambo yoyote ambayo waweza kukumbana nayo.
Elimu
Mabaraza yenyeji yaweza kutoa habari kuhusu huduma za elimu (kama vile mashule) na ambayo ni ya watoto, na pia kuhusu nafasi zinazopatikana za elimu ya watu wazima.
Kazi
Kama huna uraia wa Uingereza kwaweza kuwa na mipaka kuhusu kazi ambayo waweza kufanya. Ni muhimu kutafuta habari zaidi kuhusu jambo hili, kwa maana watu wanaopatikana wakifanya kazi bila idhini waweza kuwa katika hatari ya kufukuzwa nchini. Waweza kupata mawaidha ya bure kutoka kwa ‘Citizens Advice Bureau' (ona sehemu ya Mawaidha ya Kisheria hapa chini)
Makao
Baraza lenyeji hutoa huduma mbalimbali za makao, kwa mfano: mawaidha, orodha ya nyumba za karibu ambazo zinakodishwa, nyumba au vyumba vya ubapa, na auni
Uhamiaji
Viungo vya manufaa:
Ushauri wa Kisheria
Waweza kupata ushauri wa bure wa kisheria kutoka kwa ‘Citizen's Advice Bureau' (CAB). Kama unahitaji mkarimani waweza kupanga haya; yafaa kupiga simu na kupanga kikao kabla ya kwenda ili waweze kupanga ili mkarimani awepo. Kama waongea Kiingereza kidogo waweza kuwapigia simu, lakini kama huwezi itakubidi umuombe mtu mwenye kuongea Kiingereza kufanya hivi kwa niaba yako.
Ofisi za ‘Citizens Advice Bureau' za Riding Mashariki:
Hull Citizens Advice Bureau - (Simu) 01482 224 608
Waweza kupata mawaidha ya kisheria kutoka kwa wanasheria-kunao wengi walio Hull na Riding Mashariki. Kawaida itakubidi kulipa kwa huduma za wakili, lakini baadhi ya watu waweza kupata huduma hii bure kama wanahitimu kupata msaada wa ‘Legal Aid'. Je, unahitimu? Wakili, au ‘Citizens Advice Bureau' wataweza kusema kama wafaulu au la. Mawakili wengi huhitaji uombe kikao ili kuonana nao. Kama huongei Kiingereza kizuri, mtu mwingine aweza kuomba kikao kwa niaba yako. Wakili aweza kupanga mkalimani akawepo katika mkutano wenu kama unahitaji mmoja -kumbuka kuomba mkarimani kama unamuhitaji wakati wa kuomba kikao.
Pesa / Mifao
Mabaraza yenyeji yaweza kuto mawaidha na habari kuhusu mifao ambayo waweza kuwa unahitimu kupata.
Usalama
Uhasama wa Kinyumbani: Katika Riding ya Mashariki usaidizi kwa wateswa wa kike wa uhasama wa kinyumbani wapatikana kutoka kwa Mradi wa Makao wa Uhasama wa Kinyumbani (D-VAP) - tafadhali pigia simu Riding Mashariki ya Baraza la Yorkshire (ona hapa chini) na uliza kwa Mradi wa Makao wa Uhasama wa Kinyumbani.
| Kuweza kuwasiliana na Riding Mashariki ya Baraza la Yorkshire: tafadhali piga simu 01482 393 939 na sema tu "Swahili" ili wajue wahitaji mkarimani wa Kiswahili ili kuendelea na swala lako. |
Kuwasiliana na Baraza la Jiji la Hull: Tafadhali piga simu 01482 300 300 na sema tu "Swahili" kuonyesha yakwamba wahitaji mkarimani wa Kiswahili ili kuendelea na swala lako. |